Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro inakabiliwa na uhaba wa walimu 200 wa masomo ya sayansi. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Tuesday, February 2, 2016

Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro inakabiliwa na uhaba wa walimu 200 wa masomo ya sayansi.



Wilaya ya Same mkoani kirimanjaro  inakabiliwa na upungufu wa walimu 200 wa masomo ya sayansi katika shule za sekondari hali ambayo imesababisha wanafunzi kushindwa kufanya vizuri kitaaluma  na hivyo kuisababisha wilaya hiyo kushika nafasi ya mwisho kimkoa.
Afisa elimu sekondari wilaya ya Same Bi Happynes Laizer amesema walimu wengi wanaopangiwa kufanya kazi katika wilaya hiyo wamekuwa hawaripoti kutokana na jiografia ya wilaya hiyo kuwa na milima.
 
Amesema wanafunzi wengi wanakata tamaa kutokana na ukosefu wa walimu, wanafunzi kutembea umbali mrefu na ukosefu wa vifaa vya kufundishia hali ambayo inasababisha kiwango cha taaluma katika wilaya hiyo kuzidi kushuka kila mwaka.
 
Walimu wanasema wanafunzi walio wengi hawana utamaduni wa kujisomea kutokana na wilaya hiyo kutokuwa na maktaba, pamoja na ukosefu wa vitabu vya kutosha mashuleni hali inayochangia wanafunzi wengi kushindwa kufanya vizuri kitaaluma.
 
Nao baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kwakoko wilayani Same ambao wamepatiwa kompyuta ndogo za mkononi zenye vitabu vya kujifunzia wanasema kwa sasa wana uhakika wa kufanya vizuri kitaaluma.
 
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin