Mwekezaji alalamikia mkuu wa wilaya ya Kilosa kudharau hati ya hukumu ya mahakama kuu ya ardhi. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Tuesday, February 2, 2016

Mwekezaji alalamikia mkuu wa wilaya ya Kilosa kudharau hati ya hukumu ya mahakama kuu ya ardhi.


Mwekezaji wa shamba la kampuni ya Mees Estate katika kijiji cha Mbigiri wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro amelalamikia mkuu wa wilaya hiyo Bwana  John Henjewele kuwaruhusu wananchi kuingia kwenye shamba lake lenye ukubwa wa hekari 1500 huku akitambua mahakama kuu tayari imetoa hukumu juu ya kesi ya shamba hilo na imempa haki mwekezaji huyo.
Akizungumza na ITV meneja wa shamba hilo Bwana Patric Anthoni amessema anashangazwa na hatua ya mkuu wa wilaya ya Kilosa kushindwa kuheshimu maamuzi ya mahaka  kwa kuwaruhusu wananchi kuendelea na shughuli za kilimo katika shamba la kampuni jambo ambalo linaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
 
Nao wasimamizi wa shamba wamesema walivamiwa na kundi la wananchi wakidai kuagizwa na mkuu wa wilaya ya Kilosa kuhakikisha wanalinda shamba hilo ambapo kufuatia uvamizi huo jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia kimefika katika shamba la mwekezaji huyo na kukuta wananchi wamekwisha tawanyika na hivyo kuimarisha ulinzi katika shamba hilo.
 
Akizungumza kwa njia ya simu mkuu wa wilaya ya Kilosa Bwana John Henjewele amesema muwekezaji huyo kama ana malalamiko ya msingi afuate ngazi za kisheria ili malalamiko yake yaweze kufanyiwa kazi na sio kulalamika kwenye vyombo vya habari.
 
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin