Agizo hilo limetolewa na kaimu mkuu wa mkoa wa Simiyu, ambaye ni
mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw Ponsiano Nyami katika kikao cha baraza la
madiwani wa halmashauri ya Itilima kilichowahusisha wakuu wa idara.
Nyami amesema kuwa ni lazima mkuu huyo wa shule akamatwe na
kurejeshwa kujibu tuhuma hizo zinazomkabili kwani haiwezekani kukwamisha
juhudi zinazofanywa na wananchi za kuchangia ujenzi wa vyumba vya
maabara na kuhujumiwa na baadhi ya watumishi wa chache.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Itilima Njalu Silanga amesema
kuwa kwa kitendo hicho cha mwalimu huyo ni vema sheria ichukue mkondo
wake ili kutowakatisha tamaa wananchi kuchangia nguvu kazi.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini