Mvua
kubwa iliyonyesha jana mjini Mwanhuzi wilayani Meatu takribani masaa
mawili imesababisha kuharibu miundo mbinu ya barabara na daraja kumeguka
na kuleta adha kubwa kwa abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Mwanhuzi
kuelekea Mwanza, Shinyanga, Maswa na Bariadi na baadhi ya kulala katika
eneo hilo, huku wengine wakiwa ni wagonjwa wakiwahi hospitali na kuiomba
serikali kupitia wakala wa barabara mkoa wa Simiyu kuirejesha huduma
hiyo mapema.
ITV imeshuhudia msururu wa magari ya abiria na malori zaidi ya kumi
yaliyolala jana kutokana na kuharibika kwa barabara hiyo huku basi la
kampuni ya Hokas lililonusurika kutumbukia mtoni na kuweza kuziba
barabara hivyo kulingana na ufinyu wa barabara na kumeguka kwa kuta
ambapo kilio chao kikubwa wasafiri hao ni kuiomba serikali kuifanyia
marekebisho ya dharura barabara hiyo mapema diwani wa kata ya Mwanahuzi,
Elias Shukia amesema wananchi waliokolewa nyumba zao wanahitaji msaada
wa haraka kwani wengine kwa sasa hivi.
Aidha wananchi hao wameishauri serikali kulipanua daraja la mto huo
kwani mkubwa ambapo daraja lililowekwa ni finyu na kulingana na maji
kujaa mara kwa yamekuwa yajichimba kila kukicha.
Akiongea na ITV kwa njia ya simu meneja wa wakala wa barabara,
Tanroad mkoa wa Simiyu Albert Kenti amesema tayari ameshaandaa mitambo
na vifaa kwa ajili ya kupeleka eneo la tukio ili kuanza kazi ya
matengenezo ya barabara hiyo ili kuweza kuruhusu magari yaweze kupita.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini