
Katibu Mkuu wa Zamani wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa ametoa majibu
kuhusu taarifa zinazoandikwa kwenye baadhi ya magazeti nchini pamoja na
mitandao kuwa nyumba yake iliyoko Mbezi jijini Dar es Salaam inauzwa
baada ya kushindwa kulipa mkopo wa Benki ikidaiwa kuwa mkewe aliuchukua
na kumpa mwanaume mwingine.
Taarifa hizo zilieleza kuwa Mke wa
Dk. Slaa, Josephine alichukua mkopo wa shilingi milioni 300 katika moja
kati mabenki nchini na kushindwa kuirudisha fedha hiyo.
Dk. Slaa ambaye yuko nchini Canada
akijiendeleza kimasomo, amekanusha taarifa hizo na kueleleza kuwa yeye
na mkewe Josephine hawajawahi kuchukua mkopo katika benki yoyote nchini.
“Nataka nikuambie na uwajulishe Watanzania kwamba wala si mimi Dk. Slaa wala mke wangu, Josephine kwa wakati wowote ule hatujawahi kuchukua mkopo benki,” Dk. Slaa aliliambia gazeti la Mtanzania kwa njia ya simu.
“Tangu nitoke Bungeni sijawahi kuchukua hata senti moja benki, achilia mbali propaganda ya shilingi milioni 300.
" Hivyo, ni vizuri waliokupa taarifa wakupe undani ni benki ipi nilikopa au Josephine alikopa na ni shilingi ngapi na kwa nyaraka zipi.
"Na ni vema ukafuatilia benki husika pia kama walikuwambia ni benki gani,” Mwanasiasa huyo mkongwe alieleza.
Dk. Slaa ambaye alitangaza mwaka jana
kustaafu siasa, alisema kuwa anapanga kuchukua hatua za kisheria dhidi
ya wote walioandika habari hizo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini