JAJI MKUU OTHUMAN CHANDE ATOA SIKU SABA KWA MAHAKIMU 508 WATOE MAELEZO | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Monday, February 1, 2016

JAJI MKUU OTHUMAN CHANDE ATOA SIKU SABA KWA MAHAKIMU 508 WATOE MAELEZO



 Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo mchana , kuhusu utendaji wa mahakimu wa mahakama za hakimu mkazi, mahakama za wilaya na mahakama za mwanzo ambapo alitoa siku saba kwa mahakimu 508 watoe maelezo kwani ni wasifunguliwe mashitaka ya nidhamu na kuwajibishwa kwa kufanya kazi chini ya kiwango.
Kushoto ni Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omari Mallungu na kulia ni Jaji Kiongozi wa Tanzania, Shaban Omari Lila. Jaji Chande alitoa kauli hiyo kwenye maonyesho ya wiki ya Sheria yanayoendelea viwanja vya Mnazi Mmoja. 

  Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande, akikaribishwa kutembea mabanda mbalimbali kwenye maonesho hayo.

 Mkurugenzi Msaidizi Ukaguzi na  Maadili Mahakama ya Tanzania, Warsha Ng'humbu (kushoto), akimuelekeza jambo Balbina Mrosso (kulia), kutoka Babati mkoani Manyara aliyetembelea banda la Idara ya Malalamiko kuomba msaada wa kisheria katika maonyesho hayo
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin