Wakizungumza katika kijiji cha Msolwa na kijiji cha Namwawala
wananchi hao wametupia lawama uongozi wa wilaya ya Kilombero kwa
kuwapiga wananchi na kuwatoza faini ya shilingi elfu 50 kila mfugo
ingawa pamoja na hayo halmashauri hiyo haitaki kumaliza mgogoro huo wa
mipaka uliopo baina ya wananchi na pori Tengefu la bonde la mto
Kilombero.
Naye mwenyekiti wa kijiji cha Msolwa Bwana Salum Malila amesema
makubaliano ya wanakijiji na mradi wa ramsa walikubaliana kuacha mita 60
kutoka mipaka ya pori badala yake waliamua kuacha mita 100 ili kuepusha
migogoro lakini bado uongozi wa wilaya unaendelea kuwanyanyasa na
kwamba hawapo tayari kuona ardhi yao inamilikiwa na viongozi wachache
bila sababu.
Akijibu malalamiko ya wananchi hao mkuu wa wilaya ya Kilombero
Bwana Lefy Gembe amesema pori hilo lipo kwa mujibu wa sheria na hakuna
mtu yeyote anayeruhusiwa kufanya shughuli za kibinadamu katika eneo hilo
ingawa kuna makundi makubwa ya mifugo na mashamba mengi yawakulima na
kwamba atafanya operesheni maalumu kuhakikisha hakuna mtu yeyote
anayebaki ndani ya pori hilo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini