Kauli hizo zimesemwa na wakazi wa tarafa nne za wilaya ya Same
ambao wamepata agizo la serikali la kuwataka kufyeka miti hiyo iliyo
katika maeneo ya kuzunguka makazi yao kwa madai kuwa ni dawa za kulevya
aina ya Mirungi na wao kudai kuwa ni miti ya asili inayo julikana kama
Izengo na siyo Mirungi kama inavyo daiwa lakini pia kufyekwa kwa miti
hiyo kutachangia uharibifu mkubwa wa mazingira katika hifadhi ya msitu
wa Shengena.
Kwa upande wao watalam wa mazingira kutoka taasisi zinazo jihusisha
na uhifadhi wa mazingira wamesema serikali inapaswa kuangalia kwa
mapana maamuzi yake na kutoa elimu ya kutosha kwa jamii endepo imegundua
kuwa miti hiyo inamadhara lakini ikumbuke kuwa wilaya ya Same imewai
kukumbwa na maafa mengi yaliyo sababishwa na uharibifu wa mazingira
hivyo kuna aja ya kuulinda msitu wa Shengena kwa manufaa ya umma.
ITV ilimtafuta meneja wa wakala wa misitu kanda ya kaskazini
Cathbeth Mafupa ambaye amesema ni kweli miti hii ni ya asili lakini
inamadhara kwa binadamu wanayo tumia kama dawa za kulevya na serikali
haina mpango wa kuikata miti iliyo ndani ya msitu bali ni ile iliyo
kwenye makazi ya binadamu ambayo wameipanda kwa makusudi ya kutumia kama
dawa za kulevya ili kuepusha madhara kwa watumiaji.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini