Wafanyabiashara
na wananchi zaidi ya elfu mbili wanaotumia mnada wa mifugo katika
kijiji cha Mpeta wilayani Uvinza mkoani Kigoma wamelalamikia mnada huo
kukosa huduma muhimu ikiwemo choo, josho, maji na ofisi licha ya
halmashauri ya Uvinza na serikali kuu kukusanya ushuru kila siku yamnada
hali inayohatarisha maisha ya watu.
Wamesema mnada huo unaokusanya watu kutoka mikoa mbalimbali ya
magharibi hauna choo na kusababisha watu kujisaidia hovyo porini
sambamba na kutokuwepo kwa miundombinu muhimu, ambapo wameiomba serikali
kujenga vyoo na huduma nyingine ili kuepusha mlipuko wa magonjwa ya
kipindupindu na homa za matumbo na kwamba kijiji hakinufaiki na uwepo wa
mnada katika eneo hilo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Uvinza Mrisho Gambo ameiagiza
halmashauri ya uvinza kuhakikisha choo kinajengwa vinginevyo mnada huo
utafungwa kwa kuwa unahatarisha usalama wa wananchi na kwamba serikali
ya kijiji ianze kuwashirikisha wananchi wake na wafanyabiashara ili
kuboresha miundombinu katika mnada huo.
Mnada wa mpeta Uvinza hukusanya zaidi ya watu elfu mbili kutoka
mikoa ya Tabora, Shinyanga, Katavi na Kigoma ambao huuza na kununua
mifugo na hasa Ng’ombe.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini