Ndugu zangu,
Ulimwengu wa soka ulipatwa na mshtuko mkubwa kwenye mechi ya kufungua dimba fainali za Kombe la Dunia mwaka 2002.
Senegal ilikutana na wakoloni wao waliowatawala zamani, Ufaransa.
Na kwenye kikosi cha Ufaransa alicheza pia Patrick Vieira aliyezaliwa Senegal.
Wakiongozwa na wachezaji aina ya El Hadji Diouf, Senegal ikiwa ni mara yake ya kwanza pia kushiriki fainali hizo, ilifanya miujiza kwa kuwafunga Ufaransa kwa 1-0.
Ilikuwa ni kwenye dakika ya 30, El Hadji Diouf alimtoka beki Frank Leboeuf kwenye wingi ya kushoto, na kisha Diouf akashusha majalo kwenye goli la Ufaransa.
Mabeki wale wa Ufaransa walichanganywa na majalo yale kwa jinsi mpira ulivyokuwa unayumba angani. Emmanuel Petit na kipa wake Fabien Benitez wakapotezana. Alikotokea hakukujulikana, mshambuliaji wa Senegal, Papa Boupa Diop akapachika bao lile pekee kama inavyoonekana
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini