Mbwana Samatta, amewasili nchini Ubelgiji tayari kujiunga rasmi na Klabu ya KRC Genk inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.
Samatta aliondoka nchini juzi saa 6:00 usiku kuelekea
Ubelgiji ili kukamilisha taratibu za kujiunga na klabu hiyo mpya ya
Genk, baada ya bosi wa TP Mazembe, Moise Katumbi, kukubali kumuuza.
Meneja wa mshambuliaji huyo, Jamal Kisongo, alisema
amewasiliana na Samatta na kumweleza kwamba amefika salama na ameanza
kufuata taratibu zote ili aweze kufanya kazi nchini humo.
Alisema mara baada ya kuwasili, alitakiwa kufuatilia kibali
cha kazi ambacho kitamruhusu kufanya kazi katika klabu hiyo mpya na
muda wowote ataanza mazoezi.
“Kuhusu Hati ya Uhamisho wa Kimataifa) (ITC), Katumbi
(Moise) amemhakikishia kuituma kwa klabu hiyo, kwani kabla ya kuondoka
juzi aliongea naye na kumpa baraka zote za maisha mapya katika Klabu ya
Genk,” alisema.
Kisongo alisema kwa kuwa bosi huyo wa TP Mazembe ameridhia
kumuuza Samatta kwa Genk, siku chache zijazo anatarajia kwenda nchini
Ubelgiji kwa ajili ya kusaini mkataba ambao atafaidika nao ikiwa
mshambuliaji huyo atauzwa kwa klabu nyingine.
Samatta ambaye alitwaa tuzo ya kuwa Mchezaji Bora wa Afrika
kwa wachezaji wa ndani, alikubali kujiunga na timu ya KRC Genk na
kugomea ofa zilizotolewa na klabu za Nantes na Olympique Marseille za
Ufaransa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini