Sitaki kusikia siasa tena- Mzee Yusuph | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Monday, January 25, 2016

Sitaki kusikia siasa tena- Mzee Yusuph


Mfalme wa muziki wa taarab, Mzee Yusuph amefunguka na kusema hataki kusikia siasa wala hataki kugombea nafasi yoyote ile ya uongozi, Mzee Yusuph aliyasema haya jana kupitia kipindi cha Tam tam za Mwambao cha East Africa Radio.
Mzee Yusuph mwaka jana alikuwa na nia ya kugombea ubunge kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi katika jimbo la Fuweni Zanzibar lakini baadaye alipigwa chini kwenye kura za maoni na badala yake alikuwa akionekana kwenye kampeni za chama hicho akitoa burudani kama ambavyo wasanii wengine walikuwa wakifanya.
"Sahizi nasema ukweli kabisa sitaki kusikia kitu kinaitwa siasa, na wala mwaka 2020 siwezi kugombea nafasi yoyote ile ya uongozi labda itoke nichaguliwe tu ila mimi na siasa hapana, kwa sasa mimi nataka kuangalia masuala ya biashara niwe mfanyabiashara mkubwa kama wakina Dr Reginald Mengi, Azam, Mo Dewji yaani nataka kushindana na watu hawa kibiashara ila sio siasa sitaki kusikia kabisa". Alisema Mzee Yusuph.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin