Akizungumza wakati anazindua duka la MSD kanda ya kaskazini
lililopo katika hosipitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru naibu waziri
wa afya Dr. Hamisi Kigwangala amesema ni jambo lililoko wazi na lisilo
na shaka kuwa ubadhirifu upo na wahusika wapo hivyo ni bora yaliyoko
ndani ya bodi yakafanyika kwani hakuna njia ya mkato.
Aidha Dr Kigwangala amesema kimsingi MSD inajitahidi kufikisha dawa
kwa walaji lakini jitihada hizo haziwezi kuwa na tija kama baadhi ya
watendaji wezi na wasiowajibika wataendelea kupewa nafasi na amefafanua
na amewataka wasimamia dawa za serikali wakati serikali ikiendelea
kuhakikisha kuwa dawa zinakuwa na nembo.
Akizungumza baada ya kufunguliwa kwa duka hilo lililogharimu
milioni 47 mkurugenzi mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu, amesema kazi ya
kukabiliana na wizi wa dawa, kuchukua hatua kwa wanaohusika inaendelea
sambamba na kufungua maduka ya dawa kwenye mingine ukiwemo wa Mbeya.
Duka hilo lililofunguliwa Arusha litakuwa likihudumia mikoa ya
kanda ya kaskazini ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara zenye vituo
vya afya 919, zahanati 852. Hospitali maalum, na hospitali za rufaa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini