Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa serikali inataka bunge kibogoyo
Zitto
Kabwe amesema hayo leo kupitia mtandao wake wa Facebook, baada ya
serikali kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe.Nape Nnauye kuleta taarifa bungeni inayolenga kuzuia Televisheni ya
Taifa kurusha matangazo ya moja kwa moja ya bunge kwa madai kuwa ni
gharama kubwa.
Katika taarifa aliyotoa Waziri Nape Nnauye alidai kuwa kuanzia jana Televisheni ya Taifa itakuwa ikirusha baadhi ya vipande na haitakuwa live tena badala yake kutakuwa na kipindi maalum ambacho kitarekodi matukio ya bunge na kitakuwa kikirushwa kupitia televisheni hiyo kuanzia saa nne usiku mpaka saa tano.
Kufuatia taarifa hiyo ya waziri Nape Nnauye ambayo ilipelekea mabishano na mvutano bungeni Mbunge Zitto Kabwe amesema haya juu ya sakata hilo
"TBC walikuwa na fedha ya kurusha hotuba ya Rais 'live' ila hawana fedha ya kurusha mjadala wa hotuba hiyo! Nilisema. Dola inataka Bunge kibogoyo, Kuna wanaouliza, USA wanaonyesha Bunge 'live'? UK je? Ifahamike kuwa Nchi hizo mabunge yao yana TV na yanarusha live mikutano yao. Mpaka hapo hilo litafanyika nchini kwetu, TBC wana wajibu wa kuwapa habari wananchi. Kuzuia kurusha mikutano ya Bunge 'live' ni dalili za udikteta" Alisema Zitto Kabwe

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini