Baadhi
ya wanasiasa na wachambuzi wa mambo ya kisiasa wamemkosoa Rais John
Magufuli kwa kutohudhuria mikutano ya Kimataifa ukiwemo mkutano wa Umoja
wa Afrika (AU), uliofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia hivi karibuni
wakidai kuwa ulikuwa muhimu sana kidiplomasia.
Wameeleza
kuwa mkutano huo wa AU uliofanyika siku mbili nchini Ethiopia ulikuwa
muhimu sana kwa kuzingatia utamaduni wa mikutano hiyo kuwakaribisha
viongozi wapya wa nchi wanachama.
“Kama
Mkuu wa nchi, Rais Magufuli alipaswa kuhudhuria mkutano huo ili akutane
na viongozi wenzake na kubadilishana nao mawazo. Nadhani hayuko sahihi
kwenye hili,” Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholas Mgaya aliliambia gazeti la The Citizen.
“Kwa
namna hii, Tanzania inapoteza mengi, taswira yetu inafifia kwenye ngazi
za kimataifa. Kiongozi wetu anapaswa kuona umuhimu wa kuhudhuria kwenye
vikao kama hivyo vya kimataifa vya ngazi za juu,” aliongeza Mgaya.
Naye
mhadhiri Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Ruco) ambaye ni mtaalam wa
masuala ya kisiasa, Profesa Gaudence Mpangala aliunga mkono na kueleza
kuwa mkutano huo ulikuwa na umuhimu sana kwa Rais Magufuli kuhudhuria
akiwa na ujumbe wa viongozi wachache.
“Kama
Rais Magufuli amepanga kupunguza gharama, angeenda na watumishi
wachache. Lakini mkutano huo ulikuwa muhimu sana kwake na Taifa,” alisema Profesa Mpangala.
Hata
hivyo, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu, Gerson Msigwa alieleza
kuwa Rais Magufu alimtuma Makamo wa Rais, Bi. Samia Suluhu
kuiwakilisha nchi kwa kuwa alikuwa na majukumu mengine nchini. Kwahiyo
nchi iliwakilishwa vyema kwenye mkutano huo.
“Kama
Rais hakuhudhuria ina maana alikuwa na majukumu mengine. Lakini
aliwakilishwa na Makamo wa Rais. Kwahiyo kila kinachohusu Tanzania
kitafanyiwa kazi ipasavyo,” Msigwa aliliambia gazeti la The Citizen.
Aidha alisema kuwa bado kuna mikutano mingi ya Umoja wa Afrika mbeleni ambayo Rais Magufuli atahudhuria.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini