Katika kambi ya
wakimbizi ya Hagardera kaskazini mashariki mwa Kenya, utampata mwanamume
mfupi kwa kimo anayefuatwa sana na watoto.
Labda kwa kudhani kwamba ni mmoja wao, lakini ana tofauti kwani ana ndevu na umri wake pia ni mkubwa.Sauti yake pia ni nzito.
Huyu ni Mirr Abdullahi, mwanamume mwenye umri wa miaka 40 aliyekimbia mapigano Somalia miaka kumi iliyopita.
Amemwambia mwandishi wa BBC Bashkas Jugsodaay kwamba changamoto kuu anayokumbana nayo kambini ni kwamba watu humfanyia mzaha. Watoto pia humfuata kila aendako.
Kutokana na upweke, yeye hutumia muda wake mwingi akitafuna miraa na kuvuta sigara.
Pesa hupata kutoka kwa wahisani kambini.
Anasema akirudi huko, ana wasiwasi kwamba hali ikiwa mbaya hawezi kukimbia na kutoroka kama watu wengine.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini