Baada ya Arsenal jana kupigwa kichapo cha bao
moja mtungi na Chelsea, msanii wa bongo fleva Madee amechomoa kuchoma
gari lake kama alivyoahidi na kusema yeye hana utajiri huo wa kuchoma
gari na hata kama angekuwa nao asingeweza kufanya hivyo.
Madee
jana alipost kwenye Account yake Instgram na kudai kuwa kama Arsenal
watafungwa na Chelsea basi angechoma moja ya gari lake, lakini baada ya
kuchezea kichapo Madee amekana kuchoma gari lake moja na kusema hawezi
kufanya jambo hilo.
Kupitia Account ya Twitter leo Madee ameandika ujumbe huu "Sina utajiri huo. mpaka kufikia hatua ya kuchoma gari...na hata kama ningekua tajiri vipi. .nisingefanya upumbavu huo". Alisema Madee
Kupitia Account ya Twitter leo Madee ameandika ujumbe huu "Sina utajiri huo. mpaka kufikia hatua ya kuchoma gari...na hata kama ningekua tajiri vipi. .nisingefanya upumbavu huo". Alisema Madee
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini