Mshambuliaji wa Simba SC,Ibrahim Ajib ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi Desemba wa klabu hiyo.
Hajib
ameshinda tuzo hiyo ambayo huambatana na kitita cha Sh. 500,000 baada
ya kufunga mabao matano mwezi uliopita na kuisaidia klabu hiyo kupanda
hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara.
Kwa sasa Hajib anakosekana Simba SC kutokana na kuwa majeruhi baada ya kuumia katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar wiki iliyopita, kufuatia kugongwa na Nahodha wa zamani wa Wekundu hao wa Msimbazi,Henry Joseph.
Hajib ni moja ya wachezaji wanaopigiwa rada na klabu ya TP Mazembe ya DR Congo,kwenda kufanya majaribio.
Hadi sasa waliokwenda kwenye majaribio ni Mshambuliaji Haruna Chanongo na beki Abuu Ubwa wa Stand United.

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini