Siku moja baada ya klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji imsajili mshambuliaji
wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa anaichezea klabu ya TP Mazembe ya
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Samatta, January 30 ilishuka
dimbani ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani Cristal Arena kuikabili
klabu ya Kortrijk.Licha ya kuwa Samatta hakuwa kwenye kikosi, kwa sababu hakufanya mazoezi na timu, KRC Genk imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na mshambuliaji mwenye asili ya Zaire Christian Kabasele dakika ya 21, hizi ni taarifa na mapokezi mema kwa Samatta ambaye ndio kwanza ametua Ubelgiji kuanza maisha yake ya soka.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini