Rais Dilma Rousseff wa Brazil amekiri kwamba nchi yake imeshindwa kukabiliana na virusi vya ugonjwa hatari wa Zika.
Rais wa
Brazil ameyasema hayo Jumamosi ya jana na kuongeza kuwa maadamu mbu
wanaoeneza virusi hivyo wanaendelea kuzaliana, ni suala gumu sana kwa
serikali ya nchi hiyo kukabiliana na virusi vya Zika. Rais Rousseff
ambaye tayari ameagiza askari laki mbili na elfu 20 kwa ajili ya kutoa
mafunzo na elimu katika maeneo tofauti ya nchi hiyo juu ya namna ya
kukabiliana na ugonjwa huo, amesema maradhi hayo ni vita halisi.
Mbu
wanaoambukiza virusi vya ugonjwa wa Zika nchini Brazil, wameongezeka
mno. Kwa mujibu wa ripoti ya madaktari, ubongo wa mtoto mchanga aliyoko
tumboni, hupatwa na hitilafu baada ya mama mjamzito kung'atwa na mbu
hao. Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa, karibu watu milioni moja
wameambukizwa ugonjwa wa Zika nchini Brazil.
Virusi
vya ugonjwa huo viliibuka katika eneo kubwa la Amerika ya Latini na
katika nchi za eneo la Caribbean na sasa vinaendelea kuenea katika nchi
mbalimbali za dunia.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini