Apendekeza wakimbizi wapigwe risasi Ujerumani | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Sunday, January 31, 2016

Apendekeza wakimbizi wapigwe risasi Ujerumani

Apendekeza wakimbizi wapigwe risasi Ujerumani
Mwanasiasa mmoja mbishi nchini Ujerumani ameibua hasira kubwa, baada ya kupendekeza kuwa maafisa wa polisi wanafaa kuruhusiwa kuwapiga risasi wahamiaji, wanaojaribu kuingia nchini humo bila idhini.
Kiongozi mkuu wa chama cha mrengo wa kulia cha Alternative for Germany Frauke Petry, ameliambia gazeti la Mannheimer Morgen, kwamba anapendekeza matumizi ya silaha kwa polisi kama hatua ya mwisho.
 
Frauke Petry, wa chama cha Alternative for Germany ameliambia gazeti la Mannheimer Morgen, anapendekeza matumizi ya silaha
Sheria za polisi wa Ujerumani zinasema kuwa hakuna sheria inayodhinisha kushambulia wakimbizi kwa risasi.
Mwanachama mmoja mkuu wa chama cha Social Democrats, amemkumbusha Frauke Petry kwamba, mwanasiasa wa mwisho wa iliyokuwa Ujerumani mashariki, ambaye alimuru wakimbizi kupigwa risasi, alikuwa Erich Honecker, kiongozi mkuu wa utawala wa kikomunisti ambao ulisambaratika mwaka 1989.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin