Kamanda
wa polisi kanda maalumu Dar es salaam Simon .N. Sirro amesema jumla ya
watuhumiwa 711 wa makosa tofauti tofauti wamekamatwa kati ya siku ya
juma tatu mpaka Alhamisi usiku wiki hii.
Akitoa
taarifa kwa wanahabari leo tarehe 11 Kamanda Sirro amesema kuwa
watuhumiwa hao walikamatwa kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya unyang’anyi
wa kutumia nguvu, kukutwa na bhangi na gongo kucheza kamari,biashara za
kuuza mwili pamoja na kubugudhi abiria.
Aidha
kamanda Sirro amewataka wenyeviti wa mitaa kuwa mstari wa mbele katika
kuhakikisha kwamba maeneo yanayowazunguka yanakuwa shwari kwa
kuhakikisha hakuna biashara haramu zinazoendelea za kusababisha uhalifu.
Hata
hivyo ametaja maeneo yanayoongoza kwa kuwa na wauzaji wa bangi na gongo
katika maeneo ya Dar es salaam ni Kawe na Mabibo na kueleza kuwa
operesheni maalumu itaendelea kufanyika kila siku kuhakikisha mitaa
inakuwa safi.
Ameongeza
kwamba kwa sasa pia vijana wajulikanao kama panya road nane wamekamatwa
na kudai kuwa wanatumiwa kufanya matendo ya ki uhalifu na tajiri
mfanyabiashara wa kariakoo jijini Dar es salaam
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini