Rais John Pombe Magufuli amechukizwa na uharibifu na matumizi mabaya ya miundombinu ya mabasi ya mwendo kasi na kuagiza mamlaka zinazohusika ziwachukulie hatua kwa wasiofuata sheria.
Akiongea
wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Maktaba ya kisasa Chuo kikuu
cha Dar es Salaam, Rais John Pombe Magufuli amevitaka vyombo vya sheria
kuwachukulia hatua kali baadhi ya watu wanaohujumu miradi mbalimbali ya
maendeleo.
Akizungumza
kuhusu barabara za mwendokasi, Magufuli ametaka wayakamate magari
yanayopita kwenye barabara za mwendokasi na yapelekwe kituoni kisha
wachomolewe tairi za magari yao na yauzwe na watakuwa wamepata biashara.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini