Waziri Mkuu wa Mstaafu ambaye pia alikuwa mgombea urais kwa Tiketi ya Chadema ameibuka na kuwatakia mfungo mwema waislam wote nchini.
Kupitia ukurasa wake wa facebook. Lowassa ameandika;
"Waumini wa kiislam Tanzania wanaungana na wenzao kote duniani katika kutimiza moja ya nguzo tano Za uislam kufunga Ramadhan.
"Mwezi huu mtukufu wa Ramadhan ni kipindi muhimu sana kwa waislam kuwa karibu na mola wao.
"Kwa
niaba ya Mke wangu Regina na Mimi binafsi, nachukua nafasi hii
kuwatakia waislam wote nchini,kila la kheri na baraka tele kwenye mwezi
huu.
"Hata
hivyo nasononeshwa na hali ya maisha ya watanzania nchini hivi sasa
inavyozidi kuwa ngumu.Bei Za bidhaa mbalimbali zimezidi kupanda na zaidi
kuadimika kwa sukari ambayo ni bidhaa muhimu sana hasa katika mwezi huu
mtukufu wa Ramadhan.
"Nawaomba
wafanyabiashara kupunguza bei ya bidhaa hususan zile muhimu katika
mwezi huu, ili ndugu zetu waislam watimize Ibada yao vizuri.
"Aidha
kwa waislam nawaomba tutumie mwezi huu kuliombea taifa letu
amani,upendo na mshikamano.Lakini zaidi kuomba haki na hamu ya
watanzania kuona mabadiliko ya kisiasa yanafanyika kwa amani na wale
wenye ulevi wa kuminya haki hiyo, hawapati tena nafasi kutekeleza uovu
wao na zaidi Kuwaombea viongozi wetu wawe na hofu ya Mungu.
"Mbarikiwe sana na nawatakia kila la Kheri."
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini