Kesi
inayomkabili Isaac Abakuk ambaye anatuhumiwa kumtukana Rais John
Magufuli kwenye ukurasa wake wa facebook jana June 07 2016 ilishindwa
kuendelea kutokana na upande wa Jamhuri kutokamilisha ushahidi na
kuiomba Mahakama kuahirisha shauri hilo hadi leo June 08 2016.
Hakimu
anayesikiliza kesi hiyo Augustine Rwezire wa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Arusha alikubali ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo ambapo inatarajiwa
kuanza kusikilizwa mfululizo. Mshtakiwa anaendelea kuwa nje kwa dhamana
kusubiri kesi yake itakapotajwa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini