Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto
UNICEF limezindua ombi la dola Milioni Tisa kusaidia kudhibiti kuenea
kwa virusi vya Zika hususan Amerika ya kusini ambako virusi vimeenea
katika takribani nchi 25.
Msemaji wa UNICEF Geneva, Christophe Boulierac
UNICEF
imesema nchini Brazil, tayari inashirikiana na wadau na jamii kutuma
ujumbe wa hamasa jinsi ya kuepuka kung'atwa na mbu na kutokomeza masalia
ya wadudu hao na fedha hizo zitasaidia kupunguza makali ya madhara yake
kwa watoto wachanga , familia na ukanda mzima wa Amerika ya Kusini.
Msemaji wa UNICEF Geneva, Christopher Boulierac amewaeleza waandishi wa habari kuwa UNICEF imesisitiza umuhimu wa kuchukua hatua haraka na kuwapatia wanawake na wajawazito taarifa sahihi wanazohitaji ili kujikinga wao na watoto wao na pia kushirisha jamii jinsi ya kudhibiti kuenea kwa mbu anayebeba virusi hivyo.
Wakati huo huo WHO imesisitiza kuwa virusi vya Zika si tishio katika ujauzito kama HIV au Ebola lakini athari zake zina madhara makubwa sana kwa familia.

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini