Uuzwaji wa bidhaa za madini katika soko la nje, utalii na Serikali kuwahudumia wananchi katika sekta wezeshi kiuchumi zikiwemo ujenzi, mawasiliano, kilimo, afya na elimu ni kati ya sababu zilizotajwa kuchangia pato hilo.
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dr Albina Chuwa ametoa tathmini ya pato la Taifa katika robo ya tatu ya mwaka 2015 kuanzia Julai hadi Septemba.
Amesema licha ya pato la Taifa kuongezeka baadhi ya Sekta muhimu kwa nchi kama uzalishaji mazao ya kilimo na bidhaa za viwandani umeshuka kutokana na sababu mbalimbali.
Mkurugenzi wa Sera na Ushawishi kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Hussein Kamote anasema ukosefu wa umeme wa uhakika umeathiri kwa kiasi kikubwa Viwanda nchini.
Naye Dokta Haji Semboge , mwalimu Utafiti wa Kiuchumi katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam anaishauri Serikali kuziweka karibu Sekta za Kilimo na Viwanda kwa kuwa zinategemeana.
Pato la Taifa ni thamani ya bidhaa na huduma zilizozalishwa nchini katika kipindi husika cha mwaka, nusu mwaka au robo mwaka.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini