Mkuu
wa Ujumbe wa Shirika la Fedha Duniani, IMF, Hervé Joly amesema
Matarajio ya kiuchumi ya Tanzania yanatia matumaini sana, huku serikali
ya awamu ya tano ikiwa imeahidi kulipa malimbikizo kwa wanaotoa huduma.
Bw.Joly
amesema IMF imekamilisha tathmini ya tatu ya uchumi wa Tanzania kupitia
mfumo wa PSI,ambao mapendekezo yake yanategemewa na wahisani.
Mkuu
huyo wa IMF,amesema hali ya kiuchumi nchini Tanzania ni nzuri, na
uchumi ukiwa umekuwa kwa asilimia 7 mwaka 2015 na ongezekeo la bei za
bidhaa likiwa ni asilimia 5.6 tu.
Licha
ya hayo, amesema IMF imekuwa na wasiwasi kuhusu bajeti ya serikali
lakini amesema harakati zilizochukuliwa na serikali mpya zimetia
matumaini.
Amesema
matarajio ya ukuaji wa uchumi ni mazuri kwa mwaka 2016,huku IMF
ikipendekeza kuendelea kuleta mabadiliko katika matumizi ya serikali na
hasa kupunguza madeni ya TANESCO.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini