
Idadi
ya wakimbizi toka nchini Burundi wanaoingia nchini imezidi kuongezeka
ambapo sasa ni wastani wa wakimbizi mia 200 hadi mia 300 hupokelewa kila
siku na kusababisha serikali na mashirika yanayotoa huduma kwa
wakimbizi kuzidiwa uwezo wa kutoa huduma na hasa huduma za afya.
Hali hiyo imeelezwa na katibu tawala wa mkoa wa Kigoma Mhandisi
John Ndunguru wakati akipokea msaada wa vifaa vya kusaidia akinamama
kujifungua kutoka shirika la World Lung Foundation ambapo amesema hali
ya huduma za afya kwa wananchi na katika makambi ya wakimbizi si za
kuridhisha kutokana na idadi kubwa ya mahitaji ikilinganishwa na
wataalam na vifaa vilivyopo ambapo amesema hadi sasa mkoa una zaidi ya
wakimbizi laki moja na elfu 70 katika makambi ya Nyarugusu na Nduta.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa shirika la World Lung Foundation
nchini Dk.Nguge Mwakatundu amesema wameamua kutoa vifaa hivyo ili
kusaidia kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi na kuepusha upasuaji usio
wa lazima huku kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Kigoma Dk Fadhil Kibaya
akieleza kuwa vituo tisa vya afya vitanufaika na msaada huo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini