Mahakama Kisutu yatupilia mbali zuio la uchaguzi wa umeya. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Thursday, January 14, 2016

Mahakama Kisutu yatupilia mbali zuio la uchaguzi wa umeya.


 mahakama
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamua kutupilia mbali kesi iliyofunguliwa na mkazi wa Dar es salaam Elias Newala  ya  zuio la muda la kufanyika uchaguzi wa mameya katika Manispaa za Kinondoni na Ilala.
Kufutwa kwa kesi hiyo ni wakati muafaka kwa manispaa hizo kuwa huru kuendelea na uchaguzi ambao ulisimama kutokana na sakata hilo la uwepo wa kesi mahakamani ambayo pia mtoa maombi alifungua kesi nyingine ya kupinga utaratibu wa uendeshaji wa uchaguzi katika Manispaa za hizo.
Uamuzi wa Mahakama ya Kisutu kuifunga kesi hiyo imetokana na hali iliyooneshwa na mtoa maombi ya kutokuwa na uharaka na kesi hiyo kwa kushindwa kuwasilisha nakala zake za madai kwa muda uliotakiwa.
Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage amesema kwa kutambua umuhimu wa kesi yenyewe inagusa masilahi ya taifa na jamii kwa ujumla  ndiyo sababu kulikuwa na uharaka wa kusikilizwa kwake.
Hakimu Mwijage alibainisha kuwa Januari 8 mtoa maombi aliwasilisha maombi akiomba asikilizwe upande mmoja na kisha mahakama itoe amri ya zuio la muda la upande mmoja dhidi ya  wajibu maombi ambao ni Wakurugenzi wa Manispaa za Ilala na Kinondoni  ambao kisheria ndiyo wasimamizi wa chaguzi hizo.
Amesema kwa kuwa maombi hayo yalifunguliwa chini ya hati ya dharura wakili wa mtoa maombi, Agustino Shayo, ilikubaliana amri ya zuio la muda la kutokufanyika kwa uchaguzi huo ili kusubiri usikilizwaji wa maombi ambayo yangehusisha pande zote mbili
Hata hivyo Mtoa maombi ameiambia mahakama hana nia tena ya kuendelea na kesi hiyo kwa kuwa  uwepo wake unakwamisha shughuli nyingi za kitaifa na maendeleo kwa manispaa hizo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin